Sio kila ukisemwa lazima urudishe Neno.( kama ni mwana Mungu jiokoe msalabani; yule mkuu akaa kimya)
Sio kila ukisingiziwa lazima ujitetee.(Yesu akanyamaza kimya)
Sio kila vita lazima upigane( Daudi aliuliza matokeo ya kupigana na kushinda, isingekua na mashiko asingepigana)
Sio kila silaha inakufaa kwa kushinda vita( Daudi kombati na silaha za kijeshi ziligoma, likamfaa jiwe laini)
Sio kila uzoefu utakusaidia kumshinda adui( changanya uzoefu na mtazamo sahihi)~~~~ kama nilivyoua dubu porini ndivyo nitakavyokuua wewe na utakua chakula cha ndege wa angani.
Piga mahesabi kabla ya vita.
Usitumike kama hujui kwa nini unatimika
Usioe kama hujui kwa nini unaoa
Usiandike kama hujui kwa nini unaandika
Ukifanya hivyo utakosa nguvu ya kupigana ukikutana na maneno ya Goliathi