Wednesday, June 28, 2017

Sio kila ukisemwa lazima urudishe Neno.( kama ni mwana Mungu jiokoe msalabani; yule mkuu akaa kimya)
Sio kila ukisingiziwa lazima ujitetee.(Yesu akanyamaza kimya)
Sio kila vita lazima upigane( Daudi aliuliza matokeo ya kupigana na kushinda, isingekua na mashiko asingepigana)
Sio kila silaha inakufaa kwa kushinda vita( Daudi kombati na silaha za kijeshi ziligoma, likamfaa jiwe laini)
Sio kila uzoefu utakusaidia kumshinda adui( changanya uzoefu na mtazamo sahihi)~~~~ kama nilivyoua dubu porini ndivyo nitakavyokuua wewe na utakua chakula cha ndege wa angani.
Piga mahesabi kabla ya vita.
Usitumike kama hujui kwa nini unatimika
Usioe kama hujui kwa nini unaoa
Usiandike kama hujui kwa nini unaandika
Ukifanya hivyo utakosa nguvu ya kupigana ukikutana na maneno ya Goliathi

HAPO MWANZO
HAPO MWANZO, Mungu aliziumba mbingu na nchi.
Unajua baada ya HAPO MWANZO kuziumba mbingu na nchi na kufanya uumbaji huo siku sita hakuumba tena?
Nikatafuta wakati wa HAPO MWANZO kama Mungu aliumba meli,magari,majiko ya gesi, pete za dhahabu,mashati,suruali,viatu sikuona.
Nikatafuta baada ya HAPO MWANZO kama Mungu alitengeneza mikoba kwa kutumia ngozi za wanyama, nikakosa.
Kwa nini ubaki kwenye HAPO MWANZO? Unajua nini kilitokea baada ya HAPO MWANZO? Baada ya HAPO MWANZO Mungu akaweka uwezo wa mwanadamu kuumba vitu. NUHU akatengeneza MELI ya kwanza kabla ya Archimedes kugundua kanuni ya kuzama na kuelea kwa vitu.
Edison Thompson akaumba Bulb baada ya Mungu kuitq giza usiku. Jr Dugilo akaandika kitabu cha Ongenza uwezo, Amina Sanga akaandika Nguvu ya uthubutu, Emmanuel Makwaya Godfrey akaandika To be is to do, James Kalekwa akaandika Iandike njozi yako. Mark akatengenza Facebook
Na wewe unajua kuwa Mungu aumbi kiti cha mbao, ukitaka kiti cha mbao nenda kwa fundi seremala.
Baada ya hapo mwanzo, Mungu amekasimisha uwezo wa kutengeneza batiki ndani ya Yohana Mwaigomole na vitu vyote ndani ya mwanadamu.
Hayo yote Mungu amekupa rasilimali inaitwa AKiLi na Roho Mtakatifu(msaidizi; hafanyi kazi mpaka uanze).
HAPO ULIPO is loading.......

Leadingg News and Events

ABOUT VICTOR

VICTOR DEOGRATIOUS is the Public Figure who Inspire and Motivate Youths in Tanzania on Various youths related issues that affect the youths Potential. Also is the God fearing Man who teach and Preach the Gospel of Jesus Christ.

Contact Mr. VICTOR

Name

Email *

Message *

Contact

mobile

Copyright © VICTOR DEOGRATIAS OFFICIAL | Designed and Developed by Joel Elphas
0757755228 | Mwanza Tanzania